<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>72</hymn_number>
<title>Twendeni! Haraka! TZR72</title>
<lyrics>[V1]
 Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
 Liwe mwanga kwa nchi zilizo giza.
 Bwana alisema nendeni po pote
 Kawafundisheni mataifa yote.
 Pelekeni Injili kwa jina la Yesu.
 Upesi! Twendeni haraka!

[V2]
 Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
 La upendo wa Mungu kwa watu wote;
 Aliyeupenda sana ulimwengu
 Akamtoa Yesu Mwana wake pekee
 Kaleta wokovu, tumtangazeni.
 Upesi! Twendeni haraka!

[V3]
 Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
 La uzima kwa watu waliokufa.
 Mateka ya Shetani litafungua
 Litaponyesha na kuwapa amani.
 Twendeni upesi, tukawaokoe.
 Upesi! Twendeni haraka!</lyrics>
</song>